Mwanamuziki wa tangu zama kutoka tanzania Sam Wa Ukweli amekiri kusakwa na wanadada wakiwa na madhumuni ya kutoka katika showbiz -hivyo basi wanamtumia sana ili awape kiki.
Mwanamuziki huyu amedai kuwa ana ujio mpya na hvyo basi mafans wake wawe tayari ka vibao vitakavyotikisa afrika mashariki.hapo awali, sam a ukweli aligonga vichwa vya habari baada ya kile manager wake alichosema , kuwa upuzi wake wa kwenda kwa waganga ili aweze kurudi kwenye game.
Alipofanyiwa mahojiano na E news Kutoka Tanzania, alikua na haya ya kusema.
” Wapo wanawake wanaonifuata mastaa wanataka wawe na mimi ili tutengeneze kiki lakini sasa na mimi nakuwa naangalia inanipa nini lakini nisingependa kuwataja hewani maana naweza nikagombana nao lakini wapo wengi wengine mastaa wa Bongo movie wamenifuata wanaaniambia wanataka kutoa movie lakini kuna kitu wanataka kufanya ili kiwe tofauti kwaiyo nauliza na mimi nitapata nini maana nisije nikachafuka tu wakati mimi nina familia yangu”.