English, ENTERTAINMENT, swahili

Chidi Benz atiwa mbaroni tena kwa tuhuma za dawa za kulevya.

Mazoea yanatabu.Ni maneno ya kweli na kamwe hayakosei.Mkumbuke msanii mkongwe wa bongo fleva chidi Benz! Aliwahi kamatwa kwa tuhuma za dawa za kulevya na hata kupelekwa katika taasisi ya marekebisho kwani dawa za kulevya zilikua zimevuruga akili kupindukia. Chidi alikiri makosa, akakubali kusaidiwa lakini sasa, amegonga vichwa vya habari kwa kukamatwa kwa mara nyingine kwa tuhuma io hio ya dawa aina ya Heroine.
Kulingana na Mkuu wa kituo cha polisi mkoani Dodoma , chidi Benz alikamatwa tarehe 30 Desemba mwaka 2017 siku moja tu kabla ya sikuukuu ya mwaka mpya.
Inaonekana Jitihada za wanamuziki mbalimbali na washikadau wa tasnia ya muziki Tanzania kumsaidia zimeonekana kugonga mwamba tu.

Leave a comment